Rais Samia: Wizara ya afya ilete mpango wa kukabiliana na Uviko -19

0
207

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka wizara ya Afya kufanya tathmni na kuja na maelekezo ya kuendelea kuvaa ama kuachana na uvaaji Barakoa kwani wananchi wanaonekana kuzichoka.

Hata hivyo Rais samia ameendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari kwani ugonjwa huo bado upon a kinachoendelea ni kwamba wananchi wamekubali kuendelea kuishi na ugonjwa huo.

Akizungumza wakati wa kilele cha tamasha la sita la Siku ya Kizimkazi, Rais Samia ameitaka wizara ya Afya kufanya tathmini na kutoa muongozo kuhusiana na suala hilo

“Wakati naingia katika eneo hili nimeona kila mtu akiwa hajavaa barakoa, isipokuwa mimi na timu yangu ikabidi niivue nah ii inaonesha wananchi wamechoka kuvaa barako. Sasa wizara ya afya ifanye tathmini na kutuambia tunaendaje” amesema Rais Samia.

Hata hivyo Rais Samia amewaasa wananchi kuendelea kuchanja ili kuendelea kujilinda dhidi ya ugonjwa huo wa Uviko-19