Rais Samia Suluhu Hassan amesema ndani ya serikali kuna viongozi hawasimami kwenye nafasi zao na kufanya maamuzi.
Amesema kutochukuliana hatua kwa maslahi ya kazi kunaathiri utendaji kazi serikalini, kwa sababu aidha ni ndugu au mtu wa karibu wa kiongozi
“Watu tunakimbilia vyeo lakini hatuvifanyii kazi, tuna muhali [unajua fulani kakosea lakini unaogopa kumchukulia hatua], labda ni rafiki yangu, labda nimesoma nae, labda ni wa kwetu labda ni hivi. Nepotism [undugu] inaua mashirika”- Amesema Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia ametoa rai kwa viongozi kusimamia vema mashirika na kuchukua hatua bila kangalia ukaribu alionao kwa mtendaji.