Rais Samia: Tujiwekee akiba ya mavuno

0
201


Wakulima nchini wameaswa kutunza chakula, ili kukabiliana na uhaba wa chakula pindi unapojitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Tamasha la Bulabo mkoani Mwanza, akiwa kwenye ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

Amesema mbali na kusherehekea sikukuu ya mavuno [Bulabo] watu wawe na utamaduni wa kuweka akiba ya chakula.

“Nitoe wito kwa ndugu zangu wakulima kutunza chakula cha kutosha. Kuweka akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya matumizi yetu ya familia na tusiuze chakula nje. Chakula
kibaki ndani kwa ajili ya matumizi yetu. Itakapokuja suala la uhaba wa chakula Tanzania tuwe tumejiweka vizuri hatuna shida ya chakula”. amesisitiza Rais Samia