Rais Samia : Tamasha la Kizimkazi litumike kutangaza fursa za uchumi nchini

0
209

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kusimamia na kuhakikisha miradi ya serikali inakamilika ili kuwaletea maendeleo wananchi

Akizungumza na wananchi wa Kizimkazi katika Tamasha la Kizimkazi lililofanyika katika viwanja vya Kizimkazi dimbani, Rais Samia amesema viongozi wanapaswa kusimamia miradi ambayo haijakamilika ukiwemo mradi wa maji na kituo cha afya

Aidha akizungumzia mchango wa Tamasha la Kizimkazi, Rais Samia amesema Tamasha hilo limelenga kutoa na kuongeza fursa za kiuchumi , uwekezaji na kuhamasisha utalii kwa kuendelea kuwakaribisha wageni kutoka nje ya nchi na sehemu mbalimbali nchini

Rais Samia amesema wakati Tamasha hilo linaanzishwa kulikuwa na malengo matatu;

Kuwaleta pamoja wananchi wa kusini na kuwaunganisha watanzania wote kwa ujumla wetu

Kulinda na kudumisha mila na desturi ili kuendelea kudumisha utamaduni tulionao Watanzania

Kuhamasisha shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa za uchumi zilizopo katika wilaya wa Kusini, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar

Akimalizia hotuba yake Rais Samia amewashukuru wananchi wote nchini kwa kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa na kufanikisha zoezi la sensa ya watu kwa asilimia kubwa huku akitoa wito kwa wananchi na kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani wanaoendelea na zoezi la sensa nchi nzima