Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Taifa liko imara, na viongozi wote wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaendeleza yale yaliyoachwa na Dkt. John Magufuli.
Rais Samia ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kikubwa ambacho Watanzania wote wanapaswa kufanya kwa sasa ni kuwa na moyo wa subira na kujenga umoja na mshikamano.
Kwa mujibu wa Rais Samia, huu ni wakati kwa Watanzania wote kuondoa tofauti zao, kuwa wamoja kama Taifa, kufarijiana na kudumisha amani.
Amesema huu si wakati wa kutazama mbele kwa mashaka, si wakati wa kutazama yaliyopita, bali ni wakati wa kutazama mbele ili kujenga Tanzania mpya ambayo Dkt. Magufuli aliitamani.