Rais Samia Suluhu Hassan : Ninyi ni chachu ya maendeleo

0
155

Editor Maria Kapalasula

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Wanawake wana mchango mkubwa, na ni chachu katika kuendeleza na kuinua uchumi wa Taifa.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akiwahutubia Wanawake wa Tanzania, kupitia Wanawake wa mkoa wa Dodoma.

Amesema hakuna Taifa lolote duniani ambalo limeendelea bila Wanawake, hivyo ni vema Wanawake wakatambua kuwa wana mchango mkubwa.

Amesema Wanawake wote wa Tanzania wanatakiwa kutembea kifua mbele, kwa kuwa wao ni watu muhimu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa