Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara Uganda

0
249

Rais Samia Suluhu Hassan kesho atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe, Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Museveni na kisha Viongozi hao watahudhuria hafla na kushuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga nchini Tanzania.

Hafla ya utiaji saini mkataba huo itafanyika Ikulu mjini Entebbe na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili na kampuni zitakazotekeleza ujenzi wa mradi huo mkubwa.