Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara Misri

0
188

Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuondoka kesho nchini kuelekea nchini Misri kwa ajili ya ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ziara hiyo Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi, katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja ya diplomasia , uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.

Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja na hati saba za makubaliano kati ya nchi hizi mbili.

Ziara hiyo ya kiserikali inafuatia mwaliko wa Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi.