Rais Samia Suluhu Hassan : Dkt. Kikwete na Amani Abeid Karume walinifungulia milango

0
156

Rais Samia Suluhu Hassan amemshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya ya Kikiwete na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kwa kumuamini na kumpa nafasi mbalimbali za uongozi na kumfanya aaminike.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shukrani hizo Bungeni jijini Dodoma wakati akilihutubia Bunge.

Amesema walichokifanya viongozi hao Wastaafu ni kumtengenezea njia ya kuaminiwa na viongozi waliofuata akiwemo Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu wa awamu tano wa Tanxania , ambaye alimteua kuwa Mgombea Mwenza.