Rais Samia Suluhu Hassan: Awamu ya 5 na ya 6 ni maneno tu

0
301

Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika uongozi wake ambao ni wa awamu ya Sita hatakuwa na mambo mapya isipokuwa ni kuendeleza yale yote yaliyoanzishwa katika Serikali ya awamu ya Tano iliyoongozwa na Hayati Dkt. John Magufuli.

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa kongamano lililoandaliwa na.Viongozi wa dini kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Hayati Dkt John Magufuli na kuwaombea Viongozi wengine waliopo madarakani

Amesisitiza kuwa awamu ya tano na awamu ya sita tofauti ni maneno tu, lakini kinachofanyika sasa ni kilekile kilichoanzishwa katika awamu ya tano.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita inahakikksha inakamulisha miradi yoye ya kimkakati iliyoanzishwa katika awamu ya tano.na kubuni miradi mingine yenye maslahi kwa Taifa.

Ametaja mambo.18 yaliyoanzishwa katika Serikali ya awamu ya tano ambayo awamu ya sita itayaendeleza.

Mambo hayo ni pamoja na kupiga vita Rushwa na Ufisadi, kuhimiza uwajikaji katika utumishi wa umma na kupiga vita biashara ya dawa za kulevya.