Rais Samia Suluhu Hassan atengua uteuzi wa Chalamila

0
161

Rais Samia Suluhu Hassan atengua uteuzi wa Chalamila

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila na kufanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa wawili.

Rais pia amemteua aliyekuwa katibu tawala wa mkoa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora.

Hata hivyo Rais amefanya uhamisho wa wakuu wa mikoa wawili ambapo mkuu wa mkoa wa Mara mhandisi Robert Gabriel anahamishiwa mkoani Mwanza kuchukua nafasi ya Chalamila huku mkuu wa mkoa wa Tabora Ally Happi akihamishiwa mkoa wa Mara kuchukua nafasi ya Mhandishi Robert Gabriel.

Taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa, Rais amemteua Zuwena Omar Jiri ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Simanjiro kuwa katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Batilda Salha Buriani

Tarehe ya uapisho wa viongozi hao itatangazwa baadae.