Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kuhuzunishwa na kifo cha aliyewahi kuwa Msemaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda kilichotokea mkoani Dar es Salaam.
“Tumempoteza mwanamke hodari, mchapakazi, mbunifu, mahiri na aliyethibitisha kwa vitendo kuwa wanawake wanaweza. Nitamkumbuka kwa jinsi alivyo kwa Chama na Serikali na alivyopenda nchi yake. Mungu amuweke mahala pema peponi amina,” ameeleza kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter.