Rais Samia: Siangalii makundi katika teuzi

0
206

Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza tena kuwa haangalii makundi wala anapotoka mtu, wakati anafanya teuzi mbalimbali.

Amesema anachoangalia wakati anateua viongozi mbalimbali ni sifa za anayemteua pamoja na uwezo wake wa utendaji kazi.

Reis Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akiwaapisha wakuu wa mikoa wapya pamoja na makatibu tawala wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni.

Amesema amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kuona kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakilalamikia teuzi ambazo amekuwa akizifanya.

Rais Samia amesema kama kuna mtu ama watu wanakasirishwa na teuzi anazofanya lawama ziende kwake sababu yeye ndiye mwamuzi wa mwisho na kamwe wasilaumiwe wasaidizi wake.

Rais Samia pia amesisitiza ukusanyaji wa mapato na kuwataka viongozi aliowaapisha wakaungane na walio chini yao katika kuhimiza ukusanyaji wa mapato hayo.