Rais Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuandaa mifumo na mikakati mipya ya kupambana na vitendo vya rushwa.
Rais Samia ametoa agizo hilo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kupokea taarifa ya Mdhibiti na MKaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ile ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
Amesema pamoja na Serikali kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa, vitendo hivyo vimezidi kuendelea, hivyo ni lazima kuwe na mikakati na mifumo mipya ya kukabiliana navyo.
Rais Samia amesisititiza atakuwa imara katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa pamoja na ukusanyaji wa mapato.