Rais Samia: Mradi wa Bwawa la Nyerere utakamilika kwa mafanikio makubwa

0
175

Rais Samia Suluhu Hassan amesema atahakikisha mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere unakuwa na mafanikio ya kiuchumi na kijamii na kuwataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kujengwa kwenye ubora uliokusudiwa.

Rais Samia ameyasema hayo leo baada ya kubonyeza kitufe na kuruhusu maji ya Mto Rufiji yaanze kujaa ndani ya bwawa hilo, akieleza kuwa mradi huo ni ndoto ya Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ili liweze kuwasaidia wakulima, wafugaji na hatimaye kuzalisha umeme utakaosaidia nchi nzima

Hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 78.68 huku baadhi ya sehemu zikiwa zimekwisha kamilika kama vile daraja la kudumu, nyumba za kudumu za wafanyakazi, kukamilika kwa njia za kupitishia maji yatakayofua umeme, jumba la mitambo na kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme mkubwa wa kilovoti 400 kutoka bwawa la Julius Nyerere hadi Chalinze

Tukio hilo limeshuhudiwa na marais wastaafu akiwemo Rais wa Awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete