Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais ameandika
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina”.
Membe amefariki dunia hii leo katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam.