Rais Samia kupata chanjo ya Corona

0
233

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kupata chanjo ya UVIKO-19 ya Johnson & Johnson kesho Julai 28, 2021, Ikulu Dar es Salaam.

Tukio hilo litafanyika ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa chanjo hiyo ambayo itaanza kutolewa kwa makundi maalum wakiwemo wazee, wagonjwa, wahudumu wa sekta ya afya na makundi yaliyo mstari wa mbele.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, baada ya Rais kuchanjwa katika hafla ya uzinduzi itakayofanyika Ikulu, taratibu za kutoa chanjo kwenye vituo vilivyoandaliwa zitaanza.

Serikali ya Tanzania ilijiunga na mpango wa COVAX kwa ajili ya kupata chanjo hiyo Juni 15 mwaka huu.

Julai 24 mwaka huu Dkt. Gwajima aliongoza mapokezi ya chanjo hiyo ya dozi 1,058,400 ikiwa ni shehena ya awamu ya kwanza.