Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa baada ya kupata kura 1914 kati ya kura 1915 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM unaofanyika mkoani Dodoma.
Kwa upande wa nafasi ya Makamu Wenyeviti wa CCM, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar baada ya kupata kura 1912 kati ya kura zote 1915 zilizopigwa.
Abdulrahman Kinana yeye ametangazwa mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara baada kupata kura zote 1915 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa CCM.