Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Majaji kufanya kazi bila kuwa na upendeleo katika maamuzi yao, hasa kwenye kesi zinazowakabili Wafugaji na maeneo ya hifadhi.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu mkoani Dodoma.
Amesema kuna changamoto kwenye maeneo ya hifadhi yanayopakana na makazi ya watu ambao wengi wao ni Wafugaji, hivyo amewataka Majaji hao kusimamia haki katika maamuzi.
“Tumesikia kesi ya Lindi kwamba Wafugaji wamefanya makosa ya waziwazi, Jaji akasema nami nakwenda huko huko kutizama na kurudi na kusema hawana makosa sasa utajiuliza kuna nini hapo, sasa hiyo kesi moja ya Lindi mkuu wa Mkoa akasema sikubali niambiwe nakiuka maamuzi ya Mahakama lakini sikubali “. amesema Rais Samia.