“Jingine lililonileta tufanye mabadiliko ambalo silipendi sana ni kutokuelewana, Mawaziri na Makatibu Wakuu, Mawaziri na Manaibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu wake kuna kutokuelewana. Hadi unaona kabisa hapa kuna hatari kazi hazifanyiki inabidi ubadilishe.
Silipendi sana na nataka niwaambie nadhani hii itakuwa mara ya mwisho kutumia sababu hiyo kupangua wizara, likijitokeza tena ina maana hamuwezani na hamuwezi kufanya kazi kwa hiyo wote wawili mnakwenda.
Kama ni Katibu Mkuu na Naibu wake mtakwenda wote, Waziri na Naibu wake mtakwenda wote, Naibu na Waziri mtakwenda wote ina maana wizara imewashinda hamuwezi kufanya kazi.”
Rais Samia Suluhu Hassan