Rais Samia azindua barabara ya 8.1km Babati

0
140

Miaka minne mbele, Rais Samia Suluhu Hassan amerejea Babati mkoani Manyara kuzindua barabara yenye urefu wa kilometa 8.1 katika hatua za kukuza maendeleo katika mikoa yote ya Tanzania.

Mwaka 2018 akiwa ni Makamu wa Rais Awamu ya Tano, Rais Samia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za mji wa Babati na kurudi tena leo hii kuweka jiwe la msingi la uzinduzi rasmi wa barabara hii ambao umekamilika vyema na kukaguliwa na mkandarasi ndani ya kipindi cha makubaliano.

Akizungumza na wananchi, Rais Samia Suluhu Hassan amesema bado yapo mambo makubwa ambayo serikali yake itaendelea kufanya kwa ajili ya wananchi wa Manyara.

“Mbali na barabara, huduma nyingine za jamii; elimu, umeme, maji afya, yote tunaendelea nayo. Kazi yetu ni kutumikia wananchi, na tutawatumikia kadri Mungu atakavyo tuwezesha,” amesema.

Ujenzi wa barabara hizo umegharimu shilingi bilioni 12. Rais Samia amewaahidi Wanababati kuwa kilometa nyingine 5 za barabara zitajengwa kuuzunguka mji huu.