Rais Samia awasisitiza viongozi kuwahudumia wananchi

0
198

Rais Samia Suluhu Hassan amewasisitiza viongozi kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Njombe katika uwanja wa Sabasaba mkoani humo, ambapo amewataka viongozi kutatua kero za wananchi kabla hawajabeba mabango.

“Sikilizeni kero za wananchi, ukienda sehemu unakuta mwananchi kashika kibango halafu mnakidaka,ukiuliza unaambiwa ni kero, naombeni mkatatue.” amesema Rais Samia

Katika hatua nyingine Rais Samia amewakumbusha wananchi wa mkoa wa Njombe kushiriki kikamilifu zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

Rais Samia amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Njombe ambapo kesho ataanza ziara mkoani Iringa.