Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wakazi wa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kero ya maji, migogoro ya ardhi pamoja na kukamilisha ujenzi wa kilomita 44 za barabara zilizobaki kutoka Elerai hadi Kamwanga.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akizindua kipande cha barabara ya Sanya juu- Elerai chenye urefu wa kilomita 32.2 kilichogharimu kiasi cha shilingi bilioni 62.7.
Amesema barabara ya Sanya Juu – Kamwanga ilikuwa ni kero ya siku nyingi kwa wananchi, na hivyo amewataka wananchi kuitunza ili iweze kudumu na kuwa na manufaa kwao na watoto wao.
Awali, akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Sanya Juu – Elerai, Mtendaji Mkuu wa TANROAD, Rogatus Mativila amesema usanifu wa vipande viwili vya Bomang’ombe – Sanya Juu (24km) na Elerai – Kamwanga (44km) umekamilika na ujenzi wake utaanza hivi karibuni.
Mativila amesema ujenzi wa barabara ya Sanya Juu – Elerai ulikamilika April 29,2019 ambapo tayari mkandarasi ameshalipwa kiasi cha shilingi bilioni 45.9.