Rais Samia atunukiwa Shahada ya Juu ya Udaktari

0
76

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo kimemtunuku Shahada ya Juu ya Udaktari wa Heshima Rais Samia Suluhu Hassan, katika mahafali ya 52 duru ya tano ya chuo hicho.

Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada hiyo ya Juu ya Udaktari wa Heshima na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete.

Shahada hiyo ya Juu ya Udaktari wa Heshima imetolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya jina la Rais Samia Suluhu Hassan kupendekezwa na kuonekana kuwa anakidhi vigezo vyote vinavyotakiwa.