Rais Samia atoa pole Kenya kifo cha CDF

0
303

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Kenya Rais William Ruto, Wananchi wote wa Kenya, familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali Francis Ogolla na wanajeshi wengine tisa katika ajali ya helikopta iliyotokea katika kaunti ya Elgeyo – Marakweti.

“Natuma salamu za pole salamu za pole kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya Mheshimiwa William Ruto, wananchi wote wa Kenya, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo. Poleni sana”, ameandika Rais Samia

Ameziombea Roho za Marehemu zilale mahala pema peponi.