Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi kama ifuatavyo;
(1) Amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa – Muhimbili. Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
(2) Amemteua Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC). Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).
(3) Amemteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
(4) Amemteua Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw. Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.
(5) Amemteua Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. Bi. Fatma ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy nchini Uswis. Aidha, Bi. Fatma anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.
(6) memteua David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, teuzi hizi zinaanza mara moja.