Rais Samia ateua viongozi mbalimbali

0
183

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi za Mazao na Taasisi zinazosimamiwa na wizara ya Kilimo, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Rais amemteua Filbert Mponzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT).

Mponzi ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB.

Pia amemteua Dkt. Tausi Kida kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Dkt. Kida ni Afisa Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Victor Mwambalaswa ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB).

Mwambalaswa ni Mbunge Mstaafu na ni Meneja Mradi wa Kampuni binafsi ya Geowind Power Tanzania Limited ya Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Omar Jumanne Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pembejeo wa Taifa (AGITIF).

Bakari ni Mkurugenzi na Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzania Data Lab (dLab) ya Dar es Salaam.

Salum Hagan ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB).

Hagan ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SSC Capital ya Dar es Salaam.

Profesa Andrew Temu, yeye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA).

Profesa Temu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Trustees of the Private Agricultural Sector Support (PASS).

Abdulmajid Nsekela ameteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC).

Nsekela ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

Christopher Gachuma ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB).

Gachuma ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Nyanza Bottling Co. Ltd ya jijini Mwanza.

Uteuzi wa Wenyeviti hao umeanza tarehe 24 mwezi huu.

Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Venance Mwase kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Mwase alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Uteuzi wa Dkt. Mwase umeanza tarehe 23 mwezi huu.