Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mabalozi ambapo amemteua Meja Jenerali Ramson Mwaisaka kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Pia amemteua Meja Jenerali Paul Simuli kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mwingine aliyeteuliwa kuwa Balozi ni Mohamed Awesu ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.
Rais Samia Suluhu Hassan pia amemteua Gelasius Byakanwa kuwa Balozi, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
Dkt. Mohamed Juma Abdallah naye ameteuliwa na Rais kuwa Balozi na kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wengine walioteuliwa kuwa mabalozi ni Hassan Mwamweta (alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki), Imani Salum Njalikai (alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu, Hotuba) na Khamis Mussa Omar (alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu Ubalozi wa Tanzania Ufaransa).
Uteuzi huo wa Mabalozi umeanza Mei 10, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa.