Rais Samia ateta na Emmanuel

0
175

Mwanafunzi mwenyewe ulemavu Emmanuel Mzena anayesoma shule ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam amepata nafasi ya kuzungumza ana kwa ana na Rais Samia Suluhu Hassan na kueleza mambo yake binafsi huku Rais akiahidi kutekeleza maombi aliyowasikisha kwake.

Akiwa kwenye Ziara shuleni hapo Rais Samia amemzungumza na Emmanuel mambo kadhaa huku Rais akiweka wazi mambo mawili waliyokubaliana kwenye mazungumzo hayo mara baada kufika shuleni hapo ambayo ni swala la kuendelea kimasomo na kufungua Taasisi itakayosaidia watu wenye mahitaji kama ya Emmanuel

“Nilizungumza na Emmanuel kwa njia ya simu Kupitia TBC siku ya kuadhimisha siku yangu ya kuzaliwa na nikaahidi kuja kuwatembelea na Leo nmefanikiwa. Tumezungumza mambo kadhaa ila niwamegee mawili, kwanza ameomba kuendelea na msomo ikiwezekana nje ya Nchi, pili ameomba kufungua Taasisi itakayosaidia Watoto wengine wenye mahitaji Kama yeye. Niseme tu kuwa hayo nimemkubalia” amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia amesema Serikali imetenga shilingi milioni 704 kwaajili ya kuchapa vitabu vya sayansi na Biashara vitakavyotumiwa na wanafunzi wa kidato Cha kwanza hadi cha nne huku kukiwa na mpango wa kununua vitabu vingine kwa ajili ya kidato cha tano na sita Katika kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wa mahitaji maalum.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua vyema changamoto za wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini ndio maana Serikali inafanya kila jitihada za kuwezesha watoto kupata mahitaji kulingana na miongozo ya Kimataifa ya usawa wa kutoa elimu ngazi ya awali, msingi, Sekondari na elimu ya juu.