Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo

0
257

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, kilichotokea tarehe 08 Septemba, 2022 nchini Scotland.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais, Ikulu, Maombolezo hayo yataanza leo Septemba 10, 2022.

“Katika kipindi chote cha maombolezo, Bendera zote zitapepea nusu mlingoti zikiwemo bendera kwenye Balozi za Tanzana Duniani kote” imeeleza taarifa hiyo.