Rais Samia Suluhu Hassan, leo Mei 08, 2023 ameshiriki mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika (SADC Troika) na Nchi zinazochangia vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB), mkutano unaofanyika Windhoek, Namibia.