Rais Samia Suluhu Hassan ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania na Duniani kote kuomboleza kifo cha Baba Mtakatifu Mstaafu, Benedict XVI.
Kupitia ukurasa wa Twitter Rais Samia ameeleza kusikitishwa na kifo hicho na kutuma salamu za pole kwa Baba Mtakatifu Francisko pamoja na waumini wote wa Kanisa Katoliki.