Rais Samia ampongeza Ruto

0
260

Rais Samia Suluhu Hassan amempomgeza Rais Mteule wa Kenya, William Ruto kufuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya nchi hiyo, ambao umebariki ushindi wake.

Katika salamu zake za pongezi alizozituma kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameahidi kushirikiana na Ruto katika kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati Tanzania na Kenya ambao umedumu kwa muda mrefu.