Rais Samia amlilia Desmond Tutu

0
252

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na raia wa nchi hiyo kufuatia kifo cha Askofu Desmond Tutu.

Katika salamu zake za pole Rais Samia amesema Askofu Tutu alikuwa ni alama ya Afrika na mchango wake katika kupigania uhuru na msimamo wake kwenye amani, umoja na utawala bora utakumbukwa daima.

https://twitter.com/SuluhuSamia/status/1475351649787039748

Viongozi mbalimbali duniani wametuma salamu za pole kufuatia kifo chake ambapo miongoni mwa mambo atakayokumbukwa kwayo ni kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Tutu aliyezaliwa Oktoba 7, 1931 alifariki dunia Desemba 26, 2021 huku Cape Town, Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 90.