Rais Samia akutana na wadau wa kilimo

0
132

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo Dakar, Senegal akiwa na ujumbe wake amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegnni ambaye ni Mwenyekiti wa Africa’s Food Systems Forum (AGRF).

Pamoja na mambo mengine katika kikao hicho wamezungumzia jinsi ambavyo Tanzania imejiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kilimo utakaohudhuriwa na watu takribani elfu tatu wakiwemo viongozi, watu mashuhuri na wadau wengine wa kilimo.