Alfajiri ya leo, nchini Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan, amekamilsha uzinduzi wa filamu ya Royal Tour nchini humo.
Katika ukumbi mashuhuri wa Paramount Theatre jijini Los Angeles, California, Rais Samia ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wageni kutoka duniani na Marekani kutembelea Tanzania.
Rais Samia aliyekuwa akishangiliwa mara kwa mara na wageni waliohudhuria ukumbini hapo awali alitembelea studio za Paramount ambapo filamu na vipindi mbalimbali maarufu vya Televisheni duniani vinarekodiwa.
Rais Samia pia amepata wasaa wa kusalimiana na watu mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo akiwemo Baba mzazi wa msanii mashuhuri duniani, Rihanna, Ronald Fenty.