Rais Samia ahimiza Watanzania kuendeleza mila na desturi

0
180

Mkuu wa Machifu Tanzania (Chifu Hangaya) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongoza maelfu ya wananchi pamoja na machifu kutoka mikoa mbalimbali, kuzindua Tamasha la Utamaduni lililofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro ambalo limelenga kukuza mila na desturi za nchi ya Tanzania.

Katika hotuba yake Rais Samia, amehimiza Watanzania kukuza mila na desturi za Kitanzania ambazo zimekuwa zikisahaulika hasa kwa vijana.

“Katika kuheshimu na kuthamini na kwa nia ya kuendeleza Utamaduni wetu, Sanaa zetu na michezo pamoja na juhudi zote zilizofanywa huko nyuma na awamu zote, mimi na wenzangu tuliona haja ya kuongeza nguvu katika sekta hizi kwa kuunda wizara mahususi ya kusimamia shughuli za sanaa, Utamaduni na Michezo bila kuitishwa wizara hii jukumu jingine tulifanya hivi kwa kutambua umuhimu wa sekta hizi tatu katika kutoa ajira na kukuza uchumi wa nchi yetu lakini pia kuitangaza nchi yetu Kimataifa, tulifanya hivyo kwa kujua kwamba kiasi kikubwa maadili ya mila zetu kidogo yameacha njia kwa vijana wetu” Amesema Rais Samia

Hata hivyo Rais Samia, ametunukiwa vazi la kimila na machifu wa mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika mkoa huo.