Rais Ramaphosa atembelea kambi ya Mazimbu

0
426

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema nchi hiyo itaendelea kukumbuka juhudi za Tanzania katika kusaidia kupata ukombozi wa Taifa la Afrika Kusini.

Rais Ramaphosa amesema hayo wakati wa ziara yake katika eneo la Mazimbu mkoani Morogoro lililotumika kama kambi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini na kusema wataendelea kuwaenzi waasisi wa mataifa hayo mawili hayati Mwalimu Julius Nyerere na Nelson Mandela kwa kufanikisha kupata ukombozi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania Na Afrika Kusini hazina budi kujenga umoja na uishirikiano uliodumu kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine Rais Ramaphosa ametembelea katika eneo la makaburi walipozikwa baadhi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini.