Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamepiga Simu katika tamasha la “Orange Concert” na kuchangia Shilingi Milioni 25 kwa timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars)
Tamasha hilo lililoenzi ubunifu wa sekta za sanaa na michezo ambapo taasisi ya wasanii ya Dadahood na Baraza la Michezo Tanzania zimeungana ambapo pamoja na mambo mengine wametumia sanaa kuwachangia Twiga Stars.
Kiongozi wa kwanza kuchangia alikuwa Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa ambaye alituma ujumbe wa kuahidi kutoa Shilingi milioni 10 kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas.
Baada ya muda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan naye kupitia kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, akapiga simu na kuchangia milioni 15.