Rais Magufuli kuzindua mradi wa kihistoria wa Maji Kisarawe

0
334

Ikiwa ni muendelezo wa mikakati ya serikali ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama, Rais John Magufuli leo atazindua mradi wa Maji wa Kibamba-Kisarawe uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Mradi huu umetokana na agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Juni 21, 2017 wakati akizindua mradi wa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu.YouTube

Awamu ya kwanza ya mradi imejengwa na mkandarasi kutoka China kwa shilingi bilioni 10.6

Tanki la maji lililojengwa linauwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 6, huku mahitaji ya Mji wa Kisarawe kwa sasa yakiwa ni lita milioni 1.2 kwa siku.

Aidha, awamu ya piliitajikita kutoa maji ya ziada katika tanki la Kisarawe hadi Gongolamboto Dar es Salaam ambapo mkataba wa mradi huu ulisainiwa Mei 27, 2019. Awamu ya pili itagharimu shilingi bilioni 7.34.

Maeneo yatakayonufaika ni pamoja na Pugu, Majohe, Gongolamboto, Bangulo, Ukonga-Airwing, Kigogo pamoja na sehemu za Kinyamwezi na Kinyerezi-Tabata.