Rais Magufuli: Balozi Kijazi amewanusuru wengi wasitumbuliwe

0
221

Rais Dkt. Magufuli amesema kuna wakati alikuwa akitaka kutumbua kiongozi, lakini Balozi Kijazi alikuwa akimsihi asubiri walau siku mbili pengine huyo kiongozi atabadilika.

Amesema wapo viongozi wengi ambao sasa bado wapo madarakani na hii ni kutokana na ushauri wa Balozi Kijazi.

Amesema hata alipomaliza muda wake wa uongozi mwaka 2017, alitafuta mtu wa kushika nafasi hiyo akakosa, hivyo akamuongezea miaka miwili. Hata mwaka 2019, alipomaliza muda wake, alimuongezea tena miaka miwili, lakini sasa Mungu amemchukua akamtumikie yeye.

Ametoa pole kwa Watanzania wote na kuwataka kumtanguliza Mungu katika mambo ambayo wanaona wenyewe hawawezi kuyashinda, ikiwemo magonjwa.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Pole kufuatia Msiba wa Balozi John Kijazi hii leo katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es salaam