Rais Magufuli awataka Watanzania kutokwamishana

0
220

Watanzania wametakiwa kuacha wivu na kukwamishana katika kuleta maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Rais Dkt. John Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha Kom Food Products ambacho kimejengwa na Watanzania katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Dkt. Magufuli amempongeza muwekezaji wa kiwanda hicho ndugu Muhoja Nkwabi kwa kiwanda hicho ambacho kitazalisha vinywaji baridi, nafaka, vyakula vya mifugo na vifungashio.

“Nakupongeza sana ndugu Muhoja na umekuwa mfano wa kuigwa kuwa sisi Tanzania tunaweza kuwa na mabilionea wengi na hii ndiyo kiu yangu kuwa na wawekezaji wa viwanda vikubwa kama hivi,” amesisitiza Rais Dkt. Magufuli

Katika hatua nyingine ameweka mawe ya msingi katika jengo la utawala na jengo la wangonjwa wa nje (OPD) katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.