Rais Magufuli awasilisha fomu zake za maadili

0
179

Rais John Magufuli leo amewasilisha fomu zake za maadili katika ofisi ya Makao Makuu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi jijini Dodoma.

Katibu wa Rais Ngusa Samike amekabidhi fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili, Jaji Sivangilwa Mwangesi.

Leo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu za maadili kwa Viongozi wote kwa mujibu wa Sheria namba 13 ya mwaka 1995 ya Maadili ya Viongozi wa Umma.