Rais Magufuli atengua, nafasi kujazwa baadaye

0
174

Rais Dkt John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi Dkt Steven Nindi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo Januari 17, 2021.

Nafasi hiyo itajazwa baadaye.