Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Balozi John Kijazi kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Balozi Kijazi ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Uteuzi huu unaanza leo tarehe 21 Agosti, 2020.
. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Hayati Benjamin Mkapa.