Rais Dkt. John Magufuli amemuahidi Rais wa Jamhuri Ya Kidemokrasi Ya Congo – DRC Felix Tshisekedi kumpigia debe ili akubaliwe kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo kwa sasa ina wanachama sita.
Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo Ikulu Jijini DSM wakati wa mazungumzo na Rais Tshisekedi ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake hapa nchini.
Ziara ya Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri Ya Kidemokrasi Ya Congo –DRC hapa nchini kuthibitisha undugu kati ya nchi yake na Tanzania ambao umejikita katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, biashara na diplomasia.
Wakizungumza Ikulu Jijini DSM, Rais Dkt. John Magufuli ametoa ahadi kwa mgeni wake huyo mashuhuri kuwa atampigia chepuo
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili aweze kuingia na kunufaika na Jumuiya hiyo.
Rais Dkt. Magufuli ambaye pia amekuwa muumini mkubwa wa Lugha ya Kiswahili ambayo inakuwa kwa sasa duniani ameweka bayana makubaliano na Rais Tshisekedi kukieneza Kiswahili nchini DRC.