Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC kuachana na mtindo wa kuuza malighafi zao nje ya nchi bali waanze kuzalisha na kuuza bidhaa zilizochakatwa
Rais Magufuli ametoa wito huo wakati akifungua maonesho ya 4 ya Viwanda ya Jumuiya ya SADC yanayofanyika Jijini Dar es Salaam, na kus
ema kuwa mtindo wa kuuza malighafi hautasaidia ukuaji wa viwanda katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Dkt. Magufuli amesema, kila nchi ianze kutumia malighafi zinazopatikana katika nchi zao kuziongezea thamani ili ziwe na tija kwa viwanda vya nchi zao pamoja na kuongeza ajira.
Katika hotuba hiyo Rais Magufuli amesema, Afrika imeshindwa kupiga hatua kwa miaka mingi kutokana na mtindo huo wa kuuza malighafi badala ya kuuza bidhaa zilizochakatwa na viwanda vya ndani.
Ujumbe wa Rais Magufuli kwa Nchi Wanachama Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Alipofungua Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya SADC.
-Uwanzishwaji wa viwanda katika nchi za SADC ni mapinduzi ya lazima katika kujikomboa kiuchumi
-Kubadilisha teknolojia ya viwanda katika nchi wanachama na kuuziana malighafi miongoni mwa nchi wanachama
-Kukuza na kuendeleza ubunifu kwa kutumia teknolojia rahisi
-Kuweka miundo mbinu wezeshi ya uwanzishwaji wa viwanda pamoja na kuondoa vikwazo mipakani miongoni mwa nchi wanachama
-Kuhimiza sekta binafsi kuchangamkia fursa ya uwanzishwaji wa viwanda
-Sekta binafsi za SADC waache kulalamika na badala yake wakabiliane na changamoto za uwekezaji
-Soko la SADC ni kubwa la watu zaidi ya milioni 300 tulichangamkie.
Waandishi – Vumilia Mwasha na James Joseph Range