Rais Magufuli Aagiza:Hakuna Mwekezaji Yeyote Kukwama Kwasababu ya Kibali cha NEMC

0
298

Rais Dokta John Magufuli amewaapisha Mawaziri wawili aliowateua siku ya jumapili ya tarehe 21 ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwaapisha mawaziri hao ambao ni George Simbachawene waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira pamoja na Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe, amemwagiza waziri Simbachawene kuhakikisha kuwa hakuna mwekezaji yeyote anayekwama kuwekeza kwa sababu ya kibali cha Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

“Ni afadhali mwekezaji aanze kuwekeza kwanza alafu kibali cha NEMC kifuate”

Pia Rais Magufuli amezungumzia zao la  pamba ambapo  amesisitiza kuwa bei ya zao hilo ni 1200 huku akitoa  onyo kwa wafanyabiashara wanaowakopesha wakulima wa pamba kwa lengo kuendelea kuwadidimiza.

Pia amemtaka Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe kwenda kutekeleza nadharia na ushauri aliokuwa anatoa bungeni mara kwa mara juu ya kuendeleza kilimo  ili kukuza sekta hiyo hapa nchini

Kwa upande wake waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ameahidi kufanya kazi kwa adilifu na kuhakikisha anatatua changamoto zilizopo katika wizara hiyo pamoja na kutumia ipasavyo fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya uhifadhi wa mazingira .

Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe ameahidi kufanya kazi kadri ya uwezo wake kuhakikisha sekta ya kilimo inawainua wakulima hapa nchini.