Rais kupokea taarifa ya CAG na TAKUKURU

0
325

Rais Samia Suluhu Hassan, kesho atapokea taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na ile ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) zote za mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kwamba, hafla ya kupokea taarifa hizo itafanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.