Rais John Magufuli amesema serikali haiwezi kuiacha reli ya Tanzania

0
522

Rais John Magufuli amesema serikali haiwezi kuiacha reli ya Tanzania na Zambia kupotea kwani ni matokeo mazuri ya uongozi baina ya waasisi wa mataifa hayo mawili.

Rais Magufuli ameyasema hayo jijini Dsm katika eneo la Tazara wakati akijiandaa kwenda Rufiji kuweka jiwe la msingi wa mradi wa kufua umeme katika maporomoko ya mto Rufiji na kusema kuwa hatahakikisha reli hiyo inafanya kazi kwa ufanisi.

Pia Rais Magufuli ameitaka Menejimenti ya Tazara kutatua matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa reli hiyo.

Hapo kesho Rais Magufuli anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa kufua umeme kwenye maporomoko ya mto Rufiji.